Jasi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jasi
Remove ads

Jasi (ing.gypsum) ni madini yanayoptikana mahali pengi ambayo kikemia ni sulfati ya kalsi . Fomula yake ni CaSO4·2H2O. Ni madini laini sana yakiwa na ugumu wa 2 kwenye skeli ya Mohs. Inaweza kukwaruzwa kwa kucha.

Thumb
Jasi

Kiasili inapatikana mara nyingi kama fuwele; jasi safi haina rangi lakini ikichanganywa na madini mengine kuna fuwele za rangi kadhaa. Kwa matumizi ya kibinadamu huchomwa ikipatikana baadaye kama unga nyeupe. Unga wa jasi unaweza kuchanganywa na maji ukipokea umbo lolote baada ya kukauka tena.

Jasi imetumiwa tangu kale katika ujenzi, hasa kwenye lipu. Katika ujenzi wa kisasa bao za jasi na matofali ya jasi hutumiwa kujenga kuta za ndani zisizobeba mzigo. Kuta hizi za jasi huzuia au kuchelewesha moto ndani ya nyumba[1]. Hutumiwa pia kama dawa la kilimo na chalki ya ubao shuleni. Wasanii hutumia jasi kwa sanamu.

Remove ads

Picha

Remove ads

Marejeo

Viungo vya Nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads