Hamad bin Thuwain wa Zanzibar
Sultani wa Zanzibar From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sayyid Hamad bin Thuwain Al-Buwsaid (kwa Kiarabu: حمد بن ثويني البوسعيد; 1857 – 25 Agosti 1896) alikuwa Sultani wa tano wa Zanzibar. Alitawala Zanzibar kuanzia tarehe 5 Machi 1893 hadi 25 Agosti 1896.

Maisha
Sayyid Hamad bin Thuwaini Al-Busaid anadaiwa alizaliwa katika kisiwa cha Zanzibar mnamo mwaka 1857. Alimuoa binamu yake, Sayyida Turkia bint Turki, ambaye alikuwa binti ya Turki bin Said, Sultani wa Muscat na Oman.
Sayyid Hamad bin Thuwaini Al-Busaid alifariki ghafla tarehe 25 Agosti 1896 saa 5:40 asubuhi, ikisemekana mara baada ya kupewa sumu na binamu yake Khalid bin Barghash, ambaye alijitangaza kuwa sultani mpya. Khalid aliendelea kushikilia kiti cha enzi kwa siku tatu tu kabla ya kuondolewa na majeshi ya Waingereza katika vita vya Uingereza dhidi ya Zanzibar, vinavyotambulika kama vita vya muda mfupi kabisa katika historia.[1].
Remove ads
Medali za Heshima
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
