Kaunti ya Pokot Magharibi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kaunti ya Pokot Magharibi ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 621,241 katika eneo la km2 9,123.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 68 kwa kilometa mraba[1]..
Makao makuu yako Kapenguria.
Inajulikana kwa kuwa na bwawa la uzalishaji umeme la pekee lililo kaskazini mwa Bonde la Ufa liitwalo Turkwell. Pia, Makumbusho ya Kapenguria yapo katika kaunti hii, ambapo wapigania uhuru sita walikamatwa na kufungwa jela na serikali ya kikoloni wakati wa hali ya hatari mwaka 1952.
Remove ads
Jiografia
Kaunti ya Pokot Magharibi ina eneo la ukubwa wa km2 9 169.4 (sq mi 3 540.3). Imepakana na Uganda (magharibi), Turkana (kaskazini), Trans Nzoia na Elgeyo Marakwet (kusini) na Baringo (kusini mashariki).
Kaunti hii ina tabianchi kavu na nusu kavu. Kiwango cha mvua ni kati ya mm 400 hadi mm 1500 kila mwaka. Halijoto huwa kati ya 10 °C na 30 °C[2].
Maeneo bunge
Kaunti ya Pokot Magharibi ina maeneo bunge yafuatayo[3]:
Demografia
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]
- Kipkomo 102,633
- Pokot Central 119,016
- Pokot North 134,485
- Pokot South 80,661
- West Pokot 184,446
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads