Tarakilishi mpakato

From Wikipedia, the free encyclopedia

Tarakilishi mpakato
Remove ads

Tarakilishi mpakato, kipakatalishi, ngamizi mpakato au laptopu (kutoka Kiingereza laptop) ni aina ya tarakilishi ndogo ambayo ni rahisi kuibeba na kuitumia popote kwa shughuli mbalimbali kama vile kazi, elimu, burudani, na mawasiliano.. Watumiaji hupendelea kusafiri nazo, hususani wafanyabiashara na wanafunzi.

Thumb
Tarakilishi mpakato

Mara nyingi ina skrini, kibodi, na kipanya ndani ya kifaa kimoja, na ina uwezo wa kufanya kazi bila kuhitaji kuunganishwa na umeme kwa muda mfupi kutokana na betri yake inayoweza kuchajiwa.

Remove ads

Historia

Kipakatalishi cha kwanza kilivumbuliwa na Mwingereza mbunifu Bill Moggridge mwaka 1979. Shirika la mifumo ya GRiD lilimsaidia kuongeza ubunifu wake kwa kuweka bawaba. Mnamo mwaka 1982, vipakatalishi viliuzwa sana kwa jeshi la Marekani.

Kando ya vipakatalishi, kuna tarakilishi nyingine ndogo kama vile bapalishi au kishkwambi ambayo kwa Kiingereza inaitwa “tablet”.

Tanbihi

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads