Lugha ya kwanza
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Lugha ya kwanza ni lugha ambayo mtu anaiongea kama lugha yake ya kwanza tangu utotoni[1], umri ambamo ni rahisi zaidi kuathiriwa na mazingira na hivyo pia kujifunza kusema kama watu wa kandokando [2] .

Pia lugha hiyo huitwa lugha mama (kwa Kiingereza "mother tongue") kwa vile watu wengi hujifunza lugha yao ya kwanza kutoka kwa mama mzazi. Lakini hiyo si lazima: mara nyingine mtoto halelewi na mama, au kama analelewa, anatumia muda mrefu zaidi na watoto wenzake (hasa shuleni), hivyo anazoea lugha yao kuliko ile ya nyumbani, hata kama ni tofauti kabisa.
Kwa sababu hiyohiyo wapo watu wenye lugha mama zaidi ya moja[3].
Tarehe 17 Novemba 1999, UNESCO iliteua tarehe 21 Februari ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Lughamama.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads