MP4

From Wikipedia, the free encyclopedia

MP4
Remove ads

MP4 ni kifupi cha MPEG-4 Part 14, ambayo ni fomati ya faili ya midia inayotumika kuhifadhi video, sauti, manukuu, na metadata nyingine. Kiendelezi cha faili hii kwa kawaida huwa .mp4.

Thumb
MPEG-4 Sehemu ya 14 inapanua juu ya Umbizo Msingi la Faili la Midia la ISO (MPEG-4 Sehemu ya 12).

MP4 ni mojawapo ya fomati maarufu na zinazotumika sana kwa ajili ya kusambaza video kupitia mtandao, kwenye vifaa vya rununu, kompyuta, televisheni janja na hata mitandao ya kijamii. Hii ni kwa sababu ya ukubwa mdogo wa faili unaotokana na uwezo wake wa kutumia mbinu ya compression (kama vile H.264 au H.265), bila kupoteza sana ubora wa picha au sauti.

Faili ya MP4 ni aina ya container format, yaani hufungasha vipande mbalimbali vya data (kama video, sauti na manukuu) kwa pamoja katika faili moja. Inaruhusu sauti katika fomati kama AAC, MP3, au ALAC na video katika fomati ya MPEG-4 au H.264.

Tofauti na MP3, ambayo ni kwa sauti pekee, MP4 inaweza kushughulikia vipengele mbalimbali vya midia. Pia, ni tofauti na AVI, ambayo ni fomati ya zamani zaidi ya video na haifanyi compression kwa ufanisi sawa.

Remove ads

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads