Mana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mana (kwa Kiebrania מָן) ni chakula kilichotumiwa na Waisraeli walipotangatanga katika jangwa la Sinai miaka 40 mfululizo baada ya kutolewa na Musa nchini Misri walipokuwa wananyanyaswa.

Habari hizo zinapatikana katika vitabu vingi vya Biblia (hasa Kutoka 16:1-36 na Hesabu 11:1-9) na vilevile katika Kurani 5:27.
Pamoja na maelezo mbalimbali yaliyotolewa na wataalamu kuhusu asili ya chakula hicho, kwa imani kilitazamwa kama ishara ya pekee ya Mungu kuwashughulikia watu wake.
Yesu alikitumia hicho pia kujitambulisha ni nani kwa binadamu wote: "Mimi ndimi chakula cha kweli kilichoshuka kutoka mbinguni" (Yoh 6).
Remove ads
Fumbuzi za kisayansi
Wanasayansi wamejaribu kufumbua kitu hicho cha mana. Ufumbuzi mmoja ni kwamba mana ni sandarusi ya mchamwino, mti unaomea sana katika Rasi ya Sinai. Sandarusi hii ni tamu na ikiwa imekauka ina rangi ya hudhurungi.
Ufumbuzi mwingine ni kwamba mana ni mchozo wa wadudu kama vidukari na wadudu-gamba, k.m. mdudu-gamba wa mchamwino (Trabutina mannipara). Katika hali ya hewa moto na kavu ya Rasi ya Sinai mchozo huo hukauka haraka. Fuwele za mchozo huo ni tamu na zina rangi ya manjano au hudhurungi. Mara nyingi michozo kama huo huitwa mana pia.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads