Michael Madsen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Michael Madsen (25 Septemba 1957 – 3 Julai 2025) alikuwa mwigizaji wa filamu kutoka nchini Marekani. Anajulikana kwa michango yake katika filamu na vipindi vya televisheni. Kazi zake nyingi maarufu ni pamoja na ushirikiano wake na Quentin Tarantino.

Baadhi ya filamu zake maarufu ni pamoja na Reservoir Dogs (1992) ambapo Michael Madsen alicheza kama Mr. Blonde. Akiwa kama mmoja wa majambazi katika filamu ya kwanza ya Quentin Tarantino. Katika Thelma & Louise (1991), aliigiza kama Jimmy, mpenzi wa Thelma aliyejaribu kumsaidia baada ya matatizo yake. Katika Donnie Brasco (1997), Madsen alicheza kama Sonny Black, mwanachama wa Mafia. Madsen pia alijulikana kama Budd katika filamu Kill Bill: Vol. 1 (2003) na Kill Bill: Vol. 2 (2004), akiwa mmoja wa wauaji wa Deadly Viper Assassination Squad.
Katika Wyatt Earp (1994), Madsen aliigiza kama Virgil Earp, kaka wa Wyatt Earp. Katika Species (1995), aliigiza kama Preston Lennox, mpelelezi anayechunguza kiumbe cha kigeni. Katika Sin City (2005), alicheza kama Bob, afisa wa polisi. Katika Hell Ride (2008), alicheza kama The Gent. Katika The Hateful Eight (2015), Madsen alicheza kama Joe Gage, mmoja wa wahusika wakuu katika filamu nyingine ya Quentin Tarantino.
Remove ads
Baadhi ya filamu zake
Remove ads
Viungo vya nje
![]() |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads