Mtemi Mirambo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mtemi Mirambo (1840-1884) alikuwa mtemi wa Wanyamwezi katika magharibi ya Tanzania ya leo.

Jina lake la awali lilikuwa "Mteyla Kasanda", lakini alikuwa maarufu zaidi kama Mirambo (yaani "maiti nyingi"). Alizaliwa kama mwana wa mtemi wa Uyowa, moja kati ya maeneo madogo ya Unyamwezi akarithi utemi kutoka babake mnamo mwaka 1860.
Mirambo alitajirika kama mfanyabiashara ya pembe za ndovu na watumwa kwa njia ya misafara kati ya pwani ya Bahari Hindi na Kongo.
Alitumia sehemu kubwa ya utajiri wake kujenga jeshi la binafsi. Kwa kusudi hilo alinunua bunduki aina ya gobori na kukusanya vijana wengi walioitwa "rugaruga". Rugaruga hao walihofiwa kote. Inasemekana ya kwamba kabla ya mapigano walipewa pombe na bangi kwa kusudi la kuongeza ukatili na kupunguza hofu yao ya kifo.
Kwa kawaida vijana hao walikuwa wanaume walioishi bila ukoo na bila familia kisha kutoroka kwenye hali ya utumwa au kuwa wapagazi wa misafara.[1][2] Mirambo aliwapokea na kuwapa silaha na kwa njia hii alishinda maadui na aliweza kupanua eneo lake hadi kuwa mtemi mkuu wa Wanyamwezi[3][4] kuanzia mwaka 1860 hadi kifo chake mnamo 1884[5].
Alisifiwa na Henry Morton Stanley kama "Napoleon Bonaparte Mwafrika" kutokana na ushujaa wake dhidi ya Waarabu waliomuunga mkono Stanley mwenyewe. Hata hivyo hakufaulu kuteka Tabora kutoka mikononi mwao.
Remove ads
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads