Nabii Azaria
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Nabii Azaria (jina la Kiebrania עֲזַרְיָה, ‘Ǎzaryā, lina maana ya "YHWH amesaidia"; alizaliwa karne ya 10 KK) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale ambaye habari zake zinapatikana katika Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati sura ya 15.

Humo tunasoma kwamba, baada ya kushukiwa na Roho Mtakatifu, alikwenda kwa mfalme Asa wa Yuda kumhimiza afanye urekebisho wa kidini.
Kweli mfalme huyo alivunja sanamu za miungu na kujenga upya altare ya YHWH katika hekalu la Yerusalemu.
Baada ya hapo kulitokea kipindi cha amani kwa miaka 35.
Remove ads
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads