Nasaba ya Tang
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Nasaba ya Tang (Kichina: 唐朝; Pinyin: Táng Cháo) ilikuwa nasaba ya kifalme iliyotawala nchi ya China kuanzia mwaka 618 hadi 907 BK.

Kipindi cha Tang inahesabiwa kati ya sehemu bora ya historia ya China. Mji mkuu wa Chang'an (leo hii Xi'an) ilikuwa mji mkubwa wa dunia wakati wake ukiwa na wakazi wapatao milioni 1. Milki ya Tang ilisimamia sehemu kubwa ya barabara ya hariri na kwa njia wageni wengi walifika China. Wakati wa Tang siasa na jamii ya Kichina ilikuwa tayari kupokea wageni na kuishi nao. Hali hii ilisaidia maendeleo ya kiutamaduni. Wakati ule Ubuddha ulienea China. Vilevile wamisionari Wakristo wa kwanza walifika kutoka Uajemi wakakaribishwa na watawala.
Uchumi ulipanuka pamoja na miji. Mifereji ilichimbwa na kuwa njia za mawasiliano na kusafirisha bidhaa na mazao. Migodi zaidi ya 150 ilipeleka madini wa matumizi katika uchumi wa milki.
Sanaa mbalimbali zilistawi kama vile uchoraji, fasihi, muziki. Ufinyanzi ulifikia kiwango bora. Utawala uliboreshwa kwa kuwagawia ardhi wakulima wadogo, sheria kali mno zilifutwa na mfumo wa kodi kuboreshwa.
Kati ya teknolojia zilizobuniwa na kuanzishwa wakati wa Tang ni
- Uchapaji wa vitabu kwa njia ya pande za bao (tofauti na mbinu wa uchapaji kwa herufi za metali)
- Baruti
- ufinyanzi wa kauri
- saa ya maji
- Kiberiti
- gazeti
Wataalamu wa China wakati ule waligundua mkia wa nyotamkia na kutambua ugonjwa wa usukari.
Nguvu ya milki iliiwezesha kupanusha utawala wake juu ya maeneo makubwa ya Asia ya Mashariki na ya Kati. Katika upanuzi huo viongozi wa kijeshi waliongezeka umuhimu wakaanza kushindana kati yao. Wakubwa wa jeshi na dola walitwaa maeneo makubwa zaidi kama mali ya binafsi na tabaka ya wakulima wadogo iliharibika wakashuka chini kuwa wafanyakazi watupu mashambani. Hayo yote yalisababisha ghasia na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Mwishoni mtawala wa mwisho wa Tang alipinduliwa na jenerali wa jeshi alikamata utawala akaua watoto wote wa nasaba ya kifalme.
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Kujisomea
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads