Jimbo la Niger
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jimbo la Niger ni jimbo lililoko upande wa magharibi mwa nchi ya Nigeria na ndilo jimbo kubwa nchini humo.

Mji mkuu wake ni Minna na miji mikubwa mingine ni Bida, Kontagora na Suleja. Liliundwa mwaka wa 1976 wakati Jimbo la Kaskazini Magharibi liligawanywa na kuunda majimbo ya Sokoto na Niger.
Jina la jimbo hili linatokana na Mto Niger, mbili kati ya stesheni kubwa za kutengezea nguvu za umeme za Nigeria. Bwawa la Kainji na Bwawa la Shiroro ziko katika Jimbo hili. Pia kuna Mbuga ya Kitaifa ya Kainji iliyo kubwa zaidi nchini Nigeria na ina Ziwa Kainji.
Remove ads
Serikali
Kama majimbo mengine ya Nigeria, linaongozwa na Gavana na Bunge. Chini ya utawala wa Aliyu Mu'azu Babangida tarehe 13, Januari 2000, jimbo hili lilipitisha sheria ya Sharia kama kanuni ya sheria, ingawa idadi ya wakazi wa jimbo imekuwa kihistoria sawa kati ya Waislamu na Wakristo.
Maeneo ya Utawala

Jimbo la Niger limegawanywa katika Maeneo 25 ya Serikali za Mitaa.
|
|
|
|
|
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads