Wakarmeli Peku

From Wikipedia, the free encyclopedia

Wakarmeli Peku
Remove ads

Wakarmeli Peku (kwa Kilatini Ordo Fratrum Discalceatorum B. Mariae V. de Monte Carmelo, kifupi O.C.D.) ni watawa wa Kanisa Katoliki wanaofuata urekebisho wa shirika la Wakarmeli ulioanzishwa na Teresa wa Yesu katika karne ya 16 huko Hispania. Upande wa wanaume alisaidiwa na Yohane wa Msalaba.

Thumb
Nembo ya shirika.

Mbali ya waanzilishi hao wawili, shirika lilizaa mwalimu wa Kanisa mwingine, Teresa wa Mtoto Yesu katika karne ya 19.

Kwa jumla hao watatu wanatazamwa kuwa viongozi bora kuhusu kuzama katika sala na maisha ya kiroho kwa jumla.

Pia shirika lilizaa watakatifu na wenye heri wengi.

Mwishoni mwa mwaka 2022 shirika lilikuwa na nyumba 572 zenye watawa 3,978, (kati yao mapadri 2,897).[1]

Remove ads

Picha

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads