Patrick Garcia

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Patrick Garcia (alizaliwa kama Franz Patrick Velasco Garcia mnamo 14 Septemba 1981) ni mwigizaji wa Kifilipino, aliyejulikana sana baada ya kuigiza kama Ryan kwenye filamu iliyopata mapokezi ya hali ya juu Ufilipino, Madrasta na Nathaniel Cordero kwenye tamthiliya Darating ang umaga.

Ukweli wa haraka Amezaliwa, Kazi yake ...

Baba yake ni mhispania na mama yake ni mfilipino.

Remove ads

Maisha ya Awali

Aliwa na miaka 9, Garcia alianzia kwenye usaidizi wa kanisa la mtakatifu James Parish (Ayala), Alabang walipokuwa wakiishi. Amelitumikia kanisa kwa miaka kadhaa mpaka pale familia yake ilipohamia Frisco del Monte, Quezon City. Akiwa na miaka 13, dada yake alimshawishi kujaribu kuigiza. Alijaribu kwenye filamu ya Seprada (1994), na akapata nafasi ya kuigiza. Filamu ilikubalika na ilimtambulisha Garcia kwenye sanaa ya uigizaji nchini Ufilipino. Mwaka uliofuata, Garcia alishika nafasi tofauti-tofauti kwenye filamu na tamthiliya kama Gimik, Araw-araw, gabi-gabi, na Asero. 1996, alianza kuonja rasmi ladha ya mafanikio baada ya kujishindia tuzo ya Best Child Actor kutoka FAMAS Awards akiwa ni umri wa miaka 15, kutokana na kuigiza kama Ryan kwenye filamu Madrasta.

Baada ya Madrasta, Garcia alifanya kazi kwa juhudi, akishiriki katika nafasi zenye ushindani mkubwa katika filamu,Mano po III: My love, Nagbibinata na tamthiliya Captain Barbell, Kampanerang Kuba na Super Twins.

Remove ads

Historia yake

Patrick alikuwa mmoja kati ya waigizaji wa ‘’Ang TV’’. Baadae akaendelea akiwa mshirika wa Star Circle (sasa hivi Star Magic) kundi la pili katika ABS-CBN. Garcia ni kaka wa mwigizaji mwingine wa ‘’Ang TV’’ na Star Circle kundi la tatu, Cheska Garcia na mwanamitindo Pichon Garcia.

Patrick Garcia alianzia sanaa yake ABS-CBN na baadae akahamia GMA-7 (mahasimu wa ABS-CBN). Alipokuwa na ABS-CBN, alikuwa pamoja na Jodi Sta. Maria aliyeshirikiana naye kwenye ‘’Tabing Ilog’’, ‘’Pangako Sa’yo’’, ‘’Darating Ang Umaga’’, na ‘’Kampanerang Kuba’’ ambapo alishirikiana Anne Curtis. Mara ya mwisho alionekana kwenye ‘’Babangon Ako’t Dudurugin Kita’’ na ‘’Obra’’ za GMA-7.

Remove ads

Maisha Binafsi

Alikuwa na mahusiano ya muda mrefu na mwigizaji Jennylyn Mercado na wamebahatika kupata mtoto mmoja Agosti 2008, mtoto wao anaitwa Jazz.

Juni 2008, Patrick Garcia aliamua kwenda kutafuta maisha ng’ambo akiwa na tumaini la kujiendeleza kimasomo hasa masomo ya Directing katika chuo cha New York. Patrick aliondoka akimuacha nyuma kipenzi cha maisha yake Jennylyn Mercado, ambaye katika kipindi hicho alikuwa mjamzito.

Patrick alirudi Ufilipino kwa ajili ya harusi ya dada yake Cheska Garcia na mcheza kikapu Douglas Kramer.

Binamu zake ni Sharmaine Arnaiz na Bunny Paras.

Maigizo

Filamu

Maelezo zaidi Mwaka ...

Tamthiliya

Maelezo zaidi Mwaka ...
Remove ads

Tuzo

  • Movie Actor of the Year 14th Star Awards for Movies Batang PX
  • Best Performer Young Critics Circle Awards Batang PX
  • Best Actor Nominee FAP Awards Batang PX
  • Best Actor Nominee Urian Awards Batang PX
  • Teenage Actor of the Year Guillermo Mendoza Memorial Awards
  • Best Young Performer Parangal ng Bayan Awards
  • German Moreno Youth Achievers Awardee 46th Annual FAMAS Awards
  • Favorite Actor of the Year People's Choice Awards Batang PX
  • Best Child Actor FAMAS Awards
  • Best Supporting Actor Nominee Urian Awards
Remove ads

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads