David Massamba
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
David Massamba (jina kamili: David Phineas Bhukanda Massamba; Mkoa wa Mara, 1945 - Kurwaki, 28 Agosti 2023) alikuwa mtafiti, mchambuzi, mwandishi wa vitabu vya kitaaluma, mshauri, kiongozi na mhadhiri wa miaka mingi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha nchini Tanzania, aliyebobea kwenye fani ya lugha.[1]
Akiwa ni mtaalamu wa lugha za Kiingereza na Kiswahili, profesa Massamba alifahamika na maelfu ya wanafunzi wa elimu ya juu waliopitia mikononi mwake. Kwa upande wa Watanzania wa kawaida, profesa alijulikana kupitia kipindi kilichokuwa kikirushwa na televisheni ya Taifa cha Ulimwengu wa Kiswahili.
Remove ads
Usuli
Profesa Massamba alitokea kwenye kabila la Wakurya katika wilaya ya Musoma Vijijini.[2]
Baada ya kusoma hadi kuhitimu katika ngazi za juu za elimu, profesa Massamba akawa mhadhiri kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia miaka ya mwanzoni kabisa ya 1970.[3]
Maisha ya kikazi
Tangia alipoanza kufanya kazi chuoni UDSM, profesa Massamba hakuhamahama. Alikifanyia kazi chuo hicho huku akijiimarisha kielimu hadi kufikia ngazi ya uprofesa akibobea kwenye "Fonolojia ya Kibantu."
Profesa Massamba alifanya kazi nyingi za kukuza na kuendeleza Kiswahili. Alikuwa mmoja wa wanazuoni wa iliyokuwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili walioandaa muswada wa Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili na kamusi nyinginezo (miaka ya 80 hadi 90). Kamusi hizo zilichapishwa na kutumika.[4] Pamoja na majukumu mengi aliyokuwa nayo katika maisha yake ya kikazi, profesa alifanya kazi ya kupigiwa mfano ya uandishi wa vitabu vya kitaaluma na machapisho mengi ya aina nyingine.[5] Mifano ya kazi hizo (vitabu) ni:
- HISTORIA YA KISWAHILI: 50BK - 1500BK (Mchapishaji: Jomo Kenyatta Foundation, 2002).
- KISWAHILI: ORIGINS AND BANTU DIVERGENCE - CONVERGENCE THEORY (DSM)
- KAMUSI YA ISIMU NA FALSAFA YA LUGHA (DSM)
- FONOLOJIA YA KISWAHILI SANIFU (DSM)
Hali kadhalika alipata kuwa Mkurugenzi wa kilichokuwa Kitivo cha Mafunzo ya Kiswahili cha chuoni hapo kuanzia 1985 hadi 1991. Aliendelea kufanya kazi za uchunguzi, uchambuzi, utafiti, ufundishaji na kadhalika kwa kipindi chote cha ajira yake iliyoanzia mwanzoni mwa miaka ya 70 hadi alipostaafu miaka 50 baadae.[6]
Remove ads
Kufariki
Habari zilizowasikitisha wengi zilitangazwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa David Phineas Bhukanda Massamba, profesa mbobezi katika lugha adhimu ya Kiswahili, amefariki mnamo Agosti 28, 2023, kijijini kwake Kurwaki, kilichopo kwenye Halmashauri ya wilaya ya Musoma Vijijini, alikokuwa akiugua.[7] Kwenye shughuli ya mazishi, wananchi wenzake wakiongozwa na mbunge wao Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo, waliweka ahadi ya kujenga shule ya sekondari kwa ajili ya kumbukumbu yake itakayoitwa David Massamba Memorial Secondary School.[8]
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads