Kidhibitimbali

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kidhibitimbali
Remove ads

Kidhibitimbali (pia: kiungambali, kitenzambali na rimoti kutoka Kiing. remote control)[1] ni kifaa kinachotumiwa kudhibiti kutoka mbali vifaa vya kielektroniki kama vile televisheni, santuri ya sidii, projekta na kadhalika. Inaweza kuwasha injini inayofungua au kufunga mlango[2]. Katika tasnia hutumiwa kudhibiti vituo na mashine zinazoendeshwa pasipo mfanyakazi.

Thumb
Kidhibitimbali

Kidhibitimbali hutumiwa pia kuendesha mashine au vifaa katika mazingira ya hatari kwa binadamu, kama vile roboti zimamoto au za kusafishia mazingira yenye sumu au mnururisho.

Kitenzambali hutumia mawimbi ya infraredi au mawimbiredio kuwasiliana na vifaa lengwa[3]. Kwa kawaida hutumia betri kama chanzo cha nishati.

Vidhibitimbali hutumiwa kwa kulenga silaha na kurusha vilipukaji katika mabomu.[4]

Kwa hiyo haihitaji waya kuwasilisha amri zake. Hushikwa kwa mkono na mara nyingi huwa na vitufe kadhaa kwa kudhibiti sauti na marudio yanayoweza kuteua kituo cha runinga au redio.

Remove ads

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads