Ruby
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Ruby ni lugha ya programu ya kiwango cha juu . Iliundwa na Yukihiro Matsumoto nchini Japani na ilianzishwa tarehe 21 Desemba 1995, ikiwa na msisitizo wa urahisi, tija na usomaji wa msimbo. Lugha hii inachanganya dhana za lugha za Perl na Smalltalk, ikilenga kufanya programu ziandikwe kwa mtindo wa kimaumbile na wa kibinadamu.[1]. Iliundwa ili kurahisisha kujifunza lugha za programu. Leo tunatumia Ruby 2.7.0. Ilivutwa na Python.
Remove ads
Historia
Ilianzishwa 21 Desemba 1995 nchini Japani. Kisha kitabu cha kwanza kilichapishwa nchini Japani mwaka wa 1999; kiliitwa "Lugha ya programu Ruby inaozingatiwa kuhusu kipengee (オブジェクト指向スクリプト言語 Ruby).
Sifa Kuu
Ruby ni lugha inayotafsiriwa moja kwa moja (interpreted language) na haina haja ya kuunganishwa kabla ya kutekelezwa. Inasaidia dhana za object-oriented programming, ambapo kila kitu kinaonekana kama kitu.[2] Lugha hii pia ina urahisi wa kujumuishwa na lugha nyingine kama C na Java.
Mifumo ya Usanifu
Miongoni mwa mifumo maarufu iliyojengwa kwa Ruby ni Ruby on Rails, iliyoanzishwa mwaka 2004 na David Heinemeier Hansson. Ruby on Rails imepata umaarufu mkubwa katika ujenzi wa tovuti kwa sababu ya uwezo wake wa kurahisisha maendeleo ya programu za wavuti.[3]
Matumizi
Ruby imetumika katika kuunda programu za wavuti, programu ndogo ndogo za usimamizi, na majukwaa ya kijamii. Urahisi wake umeifanya kuvutia watengenezaji wapya na wataalamu duniani kote.[4]
Sintaksia
Sintaksia ya Ruby ni rahisi sana. Ilivutwa na sintaksia ya Pearl, lugha ya programu nyingine.
Mifano ya Ruby
Programu kwa kuchapa « Jambo ulimwengu !».
$ irb
irb(main):001:0> puts 'Jambo, Ulimwengu'
Jambo, Ulimwengu
Programu kwa kuchapa orodha ya maneno.
array = [1, 'hi', 3.14]
array.each {|item| puts item }
# prints:
# 1
# 'hi'
# 3.14
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
