Sabata
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Sabata (kwa Kitaliano: Ehi amico ... c'è Sabata, hai chiuso!, kwa haraka-haraka inatafsrika kama "Hoya washkaji... huyo ni Sabata, mmekwisha!"), ni filamu ya Spaghetti Western iliyotolewa mnamo 1969. Filamu iliongozwa na Gianfranco Parolini. Ni toleo la kwanza la Mfululizo wa Filamu za Sabata ziilizotengenezwa na Bw. Parolini, na kuchezwa na nyota Lee Van Cleef akiwa kama jina la picha. Kibwagizo cha filamu kinatoka wimbo wa mwaka 1957 ulioimbwa na Bw. Frankie Laine.
Remove ads
Hadithi
Muhtasari wa filamu
Sabata, ni mtu asiyeoongea sana akiwa na silaha mkononi, amewasili katika mji mdogo wa Texas kwenda kuzuiya wizi wa benki, na kugundua kuwa mpango huo umepangwa na vigogo wa mjini hapo, ambao walitaka kuuza mji huo kwa ajili ya njia ya reli.
Sabata akamteka kiongozi wao, Stengel, ambaye baadaye alituma wahuni kadhaa kwenda kumwangamiza Sabata, mmoja kati ya wauaji hao alikuwemo Banjo, aliitwa hivyo kwakuwa alikuwa kibeba kigizo chenye ala za muziki ambacho kilikuwa kimeficha bunduki ndani yake.
Remove ads
Washiriki
- Lee Van Cleef amecheza kama Sabata
- William Berger amecheza kama Banjo
- Ignazio Spalla amecheza kama Carrincha
- Aldo Canti amecheza kama Indio
- Franco Ressel amecheza kama Stengel
- Antonio Gradoli amecheza kama Ferguson
- Linda Veras amecheza kama Jane
- Claudio Undari amecheza kama Oswald
- Gianni Rizzo amecheza kama Judge O'Hara
Viungo vya nje
- Ehi amico... c'è Sabata, hai chiuso! at the Internet Movie Database
- (Kiingereza) Sabata katika Allmovie
- Sabata at Shobary's Spaghetti Westerns Ilihifadhiwa 17 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads