Shaha (sataranji)
kete kuu katika mchezo wa sataranji From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Shaha ni kete muhimu zaidi katika mchecho wa sataranji. Anaweza kutembea hatua 1 kila upande kwa mraba yoyote jirani. Kifupi chake katika miniti za mchezo ni "K" (kutokana Ing. "king").

Shabaha ya mchezo wa sataranji ni kumkamata shaha. Kwa hiyo ni muhimu kumlinda na kumtetea. Kama shaha anashambuliwa yaani kutishiwa moja kwa moja anapaswa kuondoka katika mraba wake kwenda mraba mwingine asipotishiwa. Kama hakuna mraba bila tishio ameshindwa na mchezo umekwisha.


Remove ads
Kuruka ngome
Kuna mwendo 1 wa pekee kama shaha na ngome hazikutembea bado na kete zote zilizopo kati yao zimeshaondoka. Hapa shaha inaruka miraba 2 kuelekea ngome na ngome inaruka upande mwingine wa shaha. Masharti ya mwendo huu ni:
- wala shaha wala ngome hazikutembea bado
- hakuna kete tena kati yao
- shaha haishambuliwi moja kwa moja
- mraba itakapofikia shaha haitishiwi wakati wa kuruka.
Tishio kwa shaha na kushindwa kwake
Kama mpinzani anaweza kuitishia kete ya shaha mshambuliwa ana njia tatu:
- Kuondoka katika mraba unaoshambuliwa kwenda mahali pasiposhambuliwa
- kukata tishio kwa kuweka kete nyingine kati ya tishio na shaha; hii haiwezekani kama mshambulizi ni kete ya farasi.
- Kupiga kete inayosababisha tishio
Kama hizi njia 3 zinashindikana upande wa shaha anayetishiwa umeshindwa na mchezo unakwisha.
Mkwamo
Mkwamo yaani hali ambako hakuna aliyeshinda unatokea kama mchezaji hana nafasi ya kutembea bila kuweka shaha kwenye mraba penye tishio ilhali haikutishiwa bado.
Remove ads
Mchezo
Wakati wa kuanza machezo wa sataranji na hadi katikati ya mchezo shaha kwa kawaida hatembei isipokuwa kuruka ngome. Mchezaji atalenga kuhifadhi shaha nyuma ya safu ya vitunda.
Lakini katika ngazi za mwishomwisho wa mchezo shaha anakuja mbele mara nyingi akishiriki katika mashambulio na katika mpango wa kubadilisha vitunda kuwa kete za nguvu zaidi.
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads