Theodori wa Canterbury
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Theodori wa Canterbury (Tarso, Kilikia, leo nchini Uturuki, 602 - Canterbury, Kent, Uingereza, 19 Septemba 690) alikuwa askofu wa jimbo kuu hilo kwa miaka 22, akiliongoza kwa nguvu ingawa mzee tayari.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Maisha
Msomi tayari, baada ya Waarabu kuteka mji wake (637) alihamia Konstantinopoli kuendelea na masomo mbalimbali, halafu mwaka 660 alihamia Roma katika monasteri ya Ukristo wa mashariki.
Papa Vitalian alimteua kuwa askofu mkuu wa Canterbury, akamweka wakfu tarehe 26 Machi 668.
Alirekebisha Kanisa la Uingereza lifuate mapokeo ya Roma akaanzisha shule ya Canterbury pamoja na Adriani wa Canterbury.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
