Tiketi

ukarasa wa maana wa Wikimedia From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Tiketi (pia: tikiti, kutoka Kiingereza "ticket") ni kipande cha karatasi au kadi inayoidhinisha mtu kuingia, kushiriki, kutumia au kusafiri. Tiketi huuzwa moja kwa moja au kidijitali siku ya matumizi au siku kadhaa kabla ya siku ya matumizi kufika.

Tiketi nyingine hushindaniwa au kutolewa bure kwa washiriki wakitimiza yanayohitajika au kama zawadi mtu anaponunua kitu au kulipa huduma fulani.

Aina za tiketi

Kuna aina nyingi za tiketi, zikiwemo:

  • Tiketi za usafiri ambazo hupewa mtu akilipa nauli kama vile tiketi za ndege, za meli, za gari la moshi na za basi za usafiri wa umma
  • Tiketi za kuhudhuria kama vile tiketi za kuhudhuria sinema, maonyesho ya kilimo, tamasha za burudani, mbuga za wanyama, makavazi, na michezo uwanjani
  • Tiketi za kushiriki kama vile michezo, mbio za kuchanga pesa,
  • Tiketi za kisiasa za kuwania viti vya kisiasa
  • Tiketi za kuegesha magari mijini
  • Tiketi za bahati na sibu
  • Tiketi za makosa ya kitrafiki
  • Tiketi za ushuru wa matumizi ya barabara (toll collection ticket)
Remove ads

Bei ya tiketi

Bei za tiketi hutofautiana kulingana na tukio. Bei ya tiketi inaweza kuamuliwa kimataifa kama vile tiketi za ndege au kuamuliwa kitaifa na serikali ya kitaifa au mkoa kama vile tiketi za maonyesho ya kilimo, za kutembelea makavazi na mbuga za wanyama na sehemu nyinginezo zinazodhibitiwa na serikali. Bei ya tiketi zingine huamuliwa na mashirika husika au watu binafsi walio na wajibu wa kupanga tamasha zile. Bei ya tiketi hudhamiriwa na vitu mingi na hubadirishwa muda kwa muda.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads