Tuzo za BAFTA
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Tuzo za Filamu za British Academy (kwa Kiing.: The British Academy Film Awards), zinazojulikana zaidi kama BAFTAs au Tuzo za BAFTA (BAFTA Awards), ni onyesho la kila mwaka la tuzo za filamu linaloandaliwa na British Academy of Film and Television Arts (BAFTA) ili kuheshimu michango bora ya Uingereza na kimataifa katika filamu. Hafla hiyo ilifanyika kwa mara ya kwanza katika sinema kuu ya Odeon (Odeon Cinema) iliyopo Leicester Square, London, kisha katika Royal Opera House kuanzia 2007 hadi 2016. Kuanzia 2017 hadi 2022, tukio hilo liliandaliwa katika Royal Albert Hall, kabla ya kuhamia Royal Festival Hall kwa mwaka wa 2023. Sanamu inayotolewa kwa washindi inaonyesha kinyago cha kisanii (theatrical mask).

Sherehe ya kwanza ya Tuzo za BAFTA ilifanyika mwaka 1949, na kwa mara ya kwanza ilitangazwa moja kwa moja kwenye BBC mwaka 1956, ikiwa na Vivien Leigh kama mtangazaji. Awali, sherehe hiyo ilikuwa ikifanyika mwezi Aprili au Mei; lakini tangu 2001, kwa kawaida hufanyika mwezi Februari.
Remove ads
Viungo vya nje
- Official website
- BAFTA Awards database Ilihifadhiwa 24 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- Museum of Broadcast Communications: BAFTA
- IMDB: BAFTA
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads