Uranusi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kuhusu matumizi ya jina Zohali kwa sayari hii tazama kipengele cha "Asili ya jina"
Remove ads
Asili ya jina
Waswahili wa kale hawakujua sayari hii. Uranusi ni jina la kimataifa lililoteuliwa katika karne ya 19 baada ya majadiliano marefu kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Ni jina la mungu wa Ugiriki ya Kale Urano (Kgi.Οὐρανός) aliyeaminiwa kuwa mungu wa anga. Lugha nyingi duniani zimepokea jina hili kwa sababu astronomia ya zamani haikujua sayari hii.
Vitabu kadhaa vinatumia jina la Kiswahili Zohali[1] [2] [3] kwa kufuata kamusi ya KAST; lakini hili ni jina la Kiswahili kwa sayari ya sita (Kng. Saturn).[4]
Remove ads
Tabia
Ni sayari kubwa ya tatu ya Mfumo wa Jua hata kama mada yake ni hasa gesi iliyoganda. Jumla ya masi yake ni mara 14 ya dunia hivyo ni sayari nyepesi kulingana na ukubwa wake. Kipenyo chake ni takriban kilomita 50,000[5].
Inazunguka Jua kwenye obiti inayochukua miaka 84. Umbali wake na Jua ni takriban mara 19 umbali wa Jua na Dunia au kilomita bilioni 2.9; afeli yake ni vizio astronomia 20.11 na periheli yake ni vizio astronomia 18.33.
Hadi mwaka 2023 miezi 27 iligunduliwa. Miezi mikubwa huitwa Miranda, Arieli, Umbrieli, Titania na Oberoni. Ina pia pete kadhaa yaani mawingu ya vumbi, barafu na mawe madogo ambayo ni nyembamba na kuzunguka sayari kwa umbo la pete. Pete za Uranusi ni hafifu kuliko zile za Zohali.
Uranusi inaonekana kama nyota hafifu sana yenye mwangaza wa 5.6 - 6. Kutokana na kuwa hafifu vile na mwendo wake wa pole hakuna utamaduni wowote wa kale ulioitambua kuwa sayari. Ilitambuliwa mara ya kwanza kuwa sayari na tarehe 13 Machi 1781 na William Herschel.
Remove ads
Tazama pia
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads