Wade Williams
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Wade Andrew William (amezaliwa tar. 24 Desemba 1961) ni mwigizaji wa filamu na tamthiliya kutoka nchini Marekani. Kkwa sasa amevaa uhusika wa nyota kwenye tamthiliya ya Prison Break ya Fox akiwa kama Captain Brad Bellick.
Remove ads
Wasifu
Maisha yake binafsi
Williams na dada zake watatu walizaliwa Georgia, na baadae wakahamia Tulsa, Oklahoma. Kama kijana, Williams alijihusisha sana na maigizo na muziki, akianzia kanisani lakini hakuipa kipaumbele sanaa ya uigizaji kama ndio msingi wa maisha yake. Baada ya kumaliza elimu ya juu, Williams alipanga kufanya maandalizi ya kujiunga na masomo ya uganga katika chuo cha Tulsa (Tulsa University). Mapenzi yake kwenye uigizaji na muziki kamwe hayakufifia na akabadilisha masomo. Williams alipata shahada katika sanaa ya maonesho na baadae akapata shahada ya pili katika sanaa ya uigizaji kutoka chuo cha Rutgers (Mason Gross School of the Arts) alipokuwa akisoma chini ya William Esper. Williams anaishi Texas akiwa na mkewe pamoja na binti yao. Kipindi akiwa chuo cha alikuwa nyota kwenye igizo Sweet Todd.
Sanaa yake
Williams alianzia maisha yake ya uigizaji Delacorte Theatre, Central Park kwenye The Taming of the Shrew akiwa na Morgan Freeman pamoja na Tracy Ulman. Pia Williams aliigiza na Denzel Washington kwenye Richard III. Williams aliendelea na shughuli zake za uigizaji mpaka ngazi ya taifa katika kazi kama vile Guys and Dolls, Les Miserables, Kiss of Spiderwoman, Ragtime na Sowboat.
Filamu zake ikiwa pamoja na Flicka, Jarhead, Colateral, Ali, na Erin Brockovich. Pia Williams ameonekana kwenye tamthilia kama Over There, Six Feet Under, Prison Break, 24, NYPD Blue, Crime Scene Investigation(CSI) na ameigiza kama Father Cronin kwenye The Bernie Mac Show.
Remove ads
Filamu alizocheza
Remove ads
Viungo vya nje
- Wade Andrew Williams at the Internet Movie Database
- Wade Williams katika Movies.com
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads