Youssou N'Dour
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Youssou N'Dour (amezaliwa 1 Oktoba, 1959) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na mwanamuziki maarufu kutoka Senegal. Anajulikana kimataifa kwa sauti yake ya kipekee na mchango wake katika muziki wa Afrika. Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni pamoja na 7 Seconds (1994) - ft. Neneh Cherry, Birima (2000), Nelson Mandela (1986), Ob-La-Di, Ob-La-Da (1995) (cover ya Beatles), Set (1990), Shaking the Tree (1990) - ft. Peter Gabriel, New Africa (1989), Medina (1997), My Hope is in You (1994) na Africa Dream Again (1996).
Remove ads
Muziki na maisha
Youssou N'Dour alianza kufanya muziki katika miaka ya 1970 akiwa kijana. Alianzisha bendi yake ya kwanza, Super Étoile de Dakar, ambayo ilichochea ukuaji wa aina ya muziki wa "Mbalax." Muziki ambao ni mchanganyiko wa muziki wa asili wa Senegal na muziki wa kisasa.
Baadaye, N'Dour alipata umaarufu ulimwenguni kwa kipawa chake cha sauti yake ya kipekee. Pia kuweza kuchanganya mitindo mbalimbali ya muziki. Aliendelea kutoa albamu nyingi zilizofanikiwa, ambazo zilimfanya awe mmoja wa wanamuziki mashuhuri kutoka Afrika.
Katika safari yake ya kumuziki, amefanikiwa kujishindia tuzo mbalilimbali. Ikiwa ni pamoja na Grammy kwa albamu zake za "Egypt" na "Rokku Mi Rokka," ambazo zilikuwa na athari kubwa kwa tasnia ya muziki wa dunia. Pia amekuwa balozi wa utamaduni wa Senegal ulimwenguni kote.
Remove ads
Siasa
Mbali na muziki, Youssou N'Dour amewahi kujihusisha sana na siasa na shughuli za kijamii nchini Senegal. Alijitupa katika kinyang'nyiro cha kuwania urais wa Senegal mwaka 2012, akigombea dhidi ya rais wa wakati huo, Abdoulaye Wade.
Diskografia
Baadhi ya albamu maarufu za Youssou N'Dour ni pamoja na:
- Immigrés (1984)
- The Lion (1989)
- Eyes Open (1992)
- Egypt (2004)
- Rokku Mi Rokka (2007)
Marejeo
- *Biography of Youssou N'Dour* - BBC News
- *Youssou N'Dour: The Voice of Senegal* - CNN
- *Official Website of Youssou N'Dour Ilihifadhiwa 21 Februari 2024 kwenye Wayback Machine.*
Viungo vya Nje
- Official Website of Youssou N'Dour Ilihifadhiwa 21 Februari 2024 kwenye Wayback Machine.
- Youssou N'Dour on YouTube
![]() |
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Youssou N'Dour kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
![]() |
Remove ads
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads