Dhamira katika fasihi ni lengo, nia au kusudio alilolikusudia msanii wa kazi ya fasihi kufikisha kwa hadhira yake. Kwa mfano, msanii anaweza kutunga wimbo ambao ukawa unajadili madhara ya pombe. Hivyo, madhara ya pombe ni dhamira ya msanii huyo. Katika fasihi, dhamira zipo za aina mbili: kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.Dhamira kuu ni lengo kuu lililomsukuma msanii wa kazi hiyo ya kifasihi kutunga kazi yake.
Dhamira ndogondogo ni malengo madogomadogo yaliyochorwa na msanii wa fasihi ili kusaidia katika kufikisha lengo kuu.