Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kama kupashana au kubadilishana mawazo, maoni, hisia au habari kwa maneno, maandishi au ishara kufikia lengo lililokubaliwa au mwelekeo uliokubaliwa (habari).
Katika mabara, lile lenye nchi nyingi zaidi ni Afrika likiwa na nchi au madola 54, likifuatiwa na bara la Ulaya likiwa na madola 48, kisha Asia likiwa na madola 44, halafu Amerika ya Kaskazini pamoja na Amerika ya Kati likiwa na madola 23, na baada yake ni Australia na Pasifiki (Oshania) likiwa na madola 14, na mwishowe ni Amerika ya Kusini likiwa na madola 12. Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 195 ulimwenguni.
Maana ya maisha ni mojawapo kati ya masuala makuu kuhusu thamani, madhumuni na umuhimu wa binadamu kuwepo duniani na wa maisha kwa jumla. Suala hilo linaweza kujitokeza katika maswali mengi tofauti yanayohusiana, kama vile Mbona tumekuwepo?, Maisha yanahusu nini? na Ni nini maana ya haya yote?