Map Graph

Milima Aberdare

Milima ya Aberdare ni safu ya milima yenye urefu wa kilomita 160 katika upande wa kaskazini wa mji mkuu wa Kenya ambao ni Nairobi na yenye wastani wa kimo wa mita 3.350 juu ya usawa wa bahari. Milima hiyo inapatikana katika sehemu ya magharibi ya kati ya Kenya, kaskazini mashariki ya Naivasha na Gilgil na kusini mwa ikweta. Milima hii hufomu sehemu ya mashariki ya Bonde la Ufa la Afrika Mashariki inayoteremka kutoka kwa tambarare ya Kinangop hadi kwa ngome ya Laikipia ambayo iko kaskazini ukielekea kusini. Upande wa mashariki, mtiririko wa maji wa milima hii huteremka ndani ya Bonde la Ufa na unaweza kuona Ziwa Naivasha na ngome ya Mau kwa mbali.

Read article
Faili:Aberdare-View_from_road_to_Ferndale.jpgFaili:Aberdare_Ranges.jpg
Nearby Places
Mlima Satima