Bonde la Wafalme
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bonde la Wafalme (kwa Kiarabu: وادي الملوك wadi al-muluk) ni bonde la huko Misri ya Kusini. Kuanzia karne ya 16 KK hadi karne ya 11 KK mafarao na wakubwa wao walizikwa huko katika makaburi yaliyochongwa kwenye miamba.[1] [2]
Bonde hilo liko kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Nile likitazama mji wa Luxor na mahekalu yake. [3] Baadhi ya wafalme waliozikwa huko ni:
- Ramses II
- Thutmose I
- Tutankhamun
Bonde hilo ni mojawapo kati ya maeneo maarufu ya akiolojia duniani. Mnamo 1979 limepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia, pamoja na makaburi yote ya eneo la Thebes ya kale (Theban Necropolis) [4] Uchunguzi, uchimbaji na uhifadhi unaendelea bondeni ukiongozwa na mamlaka ya Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni ya Misri. Kituo kipya cha watalii kimefunguliwa hivi karibuni.