Bweha au mbweha ni mojawapo wa wanyama wadogo kiasi wa familia Canidae wanaopatikana Afrika, Amerika, Asia na Ulaya na walioainishwa katika jenasi Canis, Cerdocyon, Lycalopex, Otocyon, Urocyon na Vulpes.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Bweha |
Bweha mgongo-mweusi (Canis mesomelas) |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Mammalia Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha watoto wao)
|
Oda: |
Carnivora (Wanyama mbua)
|
Nusuoda: |
Caniformia (Wanyama kama mbwa)
|
Familia: |
Canidae (Wanyama walio na mnasaba na mbwa) Fischer, 1817 |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 6; spishi 10 katika Afrika:
- Canis Linnaeus, 1758
- C. adustus Sundevall, 1847
- C. anthus Cuvier, 1820
- C. mesomelas Schreber, 1775
- Cerdocyon C.E.H. Smith, 1839
- Lycalopex Burmeister, 1854
- Otocyon Müller, 1836
- O. megalotis (Desmarest, 1822)
- Urocyon Baird, 1857
- Vulpes A. Frisch, 1775
- V. cana Blanford, 1877
- V. chama (Smith, 1833)
- V. pallida (Cretzschmar, 1827)
- V. rueppellii (Schinz, 1825)
- V. vulpes (Linnaeus, 1758
- V. zerda (Zimmermann, 1780)
|
Funga
Spishi za bweha katika jenasi Canis zina mnasaba sana na mbwa-mwitu. Kwa ukweli, siku hizi Canis anthus na Canis aureus zinafikiriwa kuwa mbwa-mwitu[1][2], lakini kwa sasa jina "bweha" litadumishwa kwa sababu linatumika sana.