David Archuleta
From Wikipedia, the free encyclopedia
David James Archuleta (amezaliwa tar. 28 Desemba 1990) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Marekani. Akiwa na umri wa miaka kumi, amepata kushinda kwenye mashindano ya kutafuta watoto wenye vipaji vya Utah Talent Competition na kuongoza kuimba kwenye mionekano mingine ya vipindi vya televisiheni. Akiwa na umri wa miaka kumi na miwili, akapata kuwa Msindi Mdogo wa Kuimba kwenye Star Search 2.[5] Mnamo mwaka wa 2007, akiwa na umri wa miaka kumi na sita, amesailiwa na kuwa mmoja kati ya waliofika fainali akiwa bwana mdogo sana kwenyue msimu wa saba wa kumtafuta mkali wa American Idol. Mnamo mwezi wa Mei 2008 amemaliza akiwa kama mgombea, na kupokea asilimia 44 za kura zaidi ya milioni 97.
David Archuleta | |
---|---|
David Archuleta mnamo Agosti 2010 | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | David James Archuleta |
Amezaliwa | 28 Desemba 1990 (1990-12-28) (umri 33)[1] Miami, Florida, Marekani |
Asili yake | Murray, Utah, Marekani |
Aina ya muziki | Pop, R&B |
Kazi yake | Mwimbaji,Mtunzi wa nyimbo, mwanafunzi |
Ala | Masauti, piano, kinanda, gitaa |
Aina ya sauti | Tenor[2][3] |
Miaka ya kazi | 2003–mpaka leo |
Studio | Jive[4] |
Tovuti | www.DavidArchuleta.com |
Mnamo mwezi wa Agosti 2008 Archuleta ametoa kibao chake kiitwacho "Crush", kibao cha kwanza kutoka kwenye albamu yake ya kwanza-yenye-jina-sawa-na-lake.[5][6][7][8] Albamu ilikuwa kutolewa miezi miwili baadaye, na kufika moja kwa moja nafasu ya pili kwenye chati za Billboard 200; na kwa mwezi wa Juni 2009, imeuza zaidi ya kopi 725,000 nchini Marekani na zaidi ya 900,000 kwa hesabu ya Dunia nzima.[9][10]