Fransisko Coll
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fransisko Coll (Gombren, 18 Mei 1812 – Vic, Barcelona, 2 Aprili 1875) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa Shirika la Wahubiri kutoka mkoa wa Catalonia, Hispania.
Baada ya kufukuzwa utawani kinyume cha haki, alidumisha imara wito wake akihubiri jina la Yesu katika mkoa huo wote.
Alianzisha shirika la Masista Wadominiko wa Kupashwa Habari Bikira Maria.
Tarehe 29 Aprili 1979 alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 11 Oktoba 2009.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Februari[1].