Frederick I Barbarossa
Mfalme Mtakatifu wa Kirumi / From Wikipedia, the free encyclopedia
Frederick I (Kijerumani: Friedrich; 1122 – 10 Juni 1190), maarufu kama Frederick Barbarossa kutokana na ndevu zake nyekundu,[1] alikuwa Kaizari ya Dola Takatifu la Kiroma kuanzia 1155 hadi kifo chake wakati wa vita vya msalaba.
Kabla ya hapo alikuwa mfalme wa Ujerumani kuanzia 1152 na mfalme wa Italia mwaka 1155.
Halafu alitiwa pia taji la mfalme wa Burgundy, huko Arles tarehe 30 Juni 1178.