Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kanisa Katoliki la Kigiriki la Romania (kwa Kiromania Biserica Română Unită cu Roma, Greco-Catolică) ni mojawapo kati ya madhehebu ya Ukristo wa mashariki yenye ushirika kamili na Papa na Kanisa Katoliki lote.
Linafuata mapokeo ya Ukristo wa Ugiriki na kutumia liturujia ya Ugiriki likiongozwa na Askofu mkuu kabisa, kwa sasa kardinali Lucian Mureşan.
Mbali ya jimbo kuu la Fǎgǎraş na Alba Iulia, nchini Romania kuna majimbo manne: Oradea Mare, Cluj-Gherla, Lugoj na Maramureş.[2]
Kanisa hilo lina pia jimbo la Mt. George huko Canton, Marekani linalowashughulikia waamini walioko Amerika Kaskazini, ikiwa ni pamoja na Canada.[3]
Kadiri ya Annuario Pontificio ya mwaka 2016, mwishoni mwa mwaka 2012 Kanisa hilo lilikuwa na waamini 504,280 katika parokia 1225, wakiongozwa na maaskofu 8 na mapadri wanajimbo 882 hivi, ingawa sensa iliyoendeshwa na serikali ya Romania mwaka 2011 ilidai waamini waliokuweko nchini walikuwa 150,593 tu.[4][5]