Leonardo da Vinci
Italian Renaissance polymath (1452−1519) / From Wikipedia, the free encyclopedia
Leonardo Da Vinci (Vinci, Toscana, Italia, 15 Aprili 1452 – Amboise, Ufaransa, 2 Mei 1519) alikuwa mtu mwenye vipaji vingi[1] kutoka nchini Italia.
'
Leonardo da Vinci | |
---|---|
Leonardo da Vinci alivyojichora | |
Amezaliwa | 15 Aprili 1452 |
Amefariki | 2 Mei 1519 |
Kazi yake | mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifuujenzi, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi |
Kifupi, alikuwa mwanahisabati, mhandisi, mwanasayansi, mgunduzi, mwanaanatomi, mchoraji, mchongaji, msanifuujenzi, mwanabotania, mwanamuziki na mwandishi.
Ndiye mwakilishi bora wa tapo la Renaissance.
Leonardo alikuwa mdadisi wa kila kitu asilia. Alitaka kujua kila kitu kinavyofanya kazi. Alikuwa hodari sana katika kusoma, kuunda na kutengeneza vitu vya aina mbalimbali tena vya kupendeza.[2]
Mwanahistoria wa sanaa Helen Gardner alisema hakuna mtu aliyewahi kuwa kama yeye kwa sababu alikuwa na shauku na vitu vingi sana: "...Akili yake na utu wake vinaonekana kuwa zaidi ya mtu, ni mtu wa ajabu na tofauti".
Leonardo siku zote alikuwa akifiria kugundua mambo mapya. Vitu vingi alivyogundua havikuwahi kufanywa. Hata hivyo, tunajua fikra zake, kwa sababu aliweka kwenye vijitabu na kuandika na kuvichora mara kwa mara.
Baadhi ya nadharia alizofikiria ni pamoja na helikopta, kifaru, baiskeli, kikokotoo, roboti na vifaa vinavyogeuza nishati ya jua kuwa umeme.
Leonardo aliweza kufanya vitu vya aina nyingi vya kijanja, lakini alikuwa maarufu sana kama mchoraji. Watu wengi hufikiria kwamba Leonardo alikuwa mmoja kati ya wachoraji bora wa historia yote. Amefanya michoro mingi sana. Miongoni mwa picha zake, mbili zilizo maarufu zaidi duniani ni Mona Lisa na Karamu ya mwisho.
Mchoro mwingine unaojulikana sana ni Vitruvian Man. Unajulikana sana hata Homer Simpson na Garfield ambazo zilichorwa kwa mraba na mzunguko ili kuonekana kama mchoro.