Mshambuliaji
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mshambuliaji (kutoka kitenzi “kushambulia”) ni mchezaji wa nafasi ya mbele anayetakiwa kufunga goli katika michezo mbalimbali kama vile: mpira wa miguu, raga, hoki ya ugani. Hivyo anacheza karibu na goli la timu pinzani akiwa na majukumu makubwa ya kufungia timu yake.
Nafasi yake uwanjani na kazi ndogo ya ukabaji awapo michezoni humaanisha mshambuliaji ndiye wa kufunga magoli mengi zaidi kwa niaba ya timu nzima na wachezaji wenzake.
Mfumo wa kisasa kwa ujumla hutumia mshambuliaji mmoja mpaka watatu; kwa mfano, mfumo uliozoeleka wa 4–2–3–1 hutumia mshambuliaji mmoja.[1][2][3]