Mshigi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mishigi, shigi au sigi ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika, Asia na Australia. Takriban spishi zote za Afrika ni ndege weusi au kahawia na weupe wenye pengine sehemu za rangi kali kama nyekundu, machungwa na njano. Spishi nyingi za Asia na Australia zina rangi kali kwa kipande kikubwa cha mwili. Ndege hawa hula mbegu hasa na wadudu pia, hususa makinda. Tago lao ni tufe la manyasi lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 4-7.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Mshigi | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mshigi kinyago-chekundu | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 8:
| ||||||||||||
Funga