Simproniani na wenzake
From Wikipedia, the free encyclopedia
Simproniani na wenzake Klaudio, Nikostrati, Kastori na Simplisi (walifariki kwenye mto Sava, Panonia, leo nchini Kroasya, 306 hivi) walikuwa wachongamawe (isipokuwa Simplisi) waliouawa katika dhuluma ya Dola la Roma kwa sababu walikataa kuchonga sanamu ya mungu Eskulapi.
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.