Skizofrenia
Shida ya akili / From Wikipedia, the free encyclopedia
Skizofrenia ni ugonjwa wa akili unaosababisha fikira na hisia zisizo za kawaida.[1] Watu wengi walio na ugonjwa huo husikia yasiyokuwemo (kama kuota njozi), na woga na makisio yasiyoeleweka (paranoia), pia wanaweza kuamini mambo ya kiajabu na yasiyoeleweka, kuzungumza bila mantiki n.k. Watu hawa huwa na ugumu wa kuhusiana na wengine inavyofaa au kudumisha kazi.
Schizophrenia | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Psychiatry, saikolojia ya Kimatibabu ![]() |
ICD-10 | F20. |
ICD-9 | 295 |
OMIM | 181500 |
DiseasesDB | 11890 |
MedlinePlus | 000928 |
eMedicine | med/2072 emerg/520 |
MeSH | F03.700.750 |
Dalili kwa kawaida huanza katika ujana baada ya umri wa miaka 16. Takriban asilimia 0.3 hadi 0.7 ya idadi ya watu duniani watakuwa na hali hiyo wakati mmoja maishani mwao.[2] Mwenendo unaoonekana na matukio yaliyoripotiwa husaidia kubaini iwapo mtu ana ugonjwa huo.
Vipengele kadhaa muhimu vinaweza kusababisha skizofrenia. Vipengele hivi ni pamoja na uhusiano wa kijamii na mtu aliye na hali hii, mazingira ya hapo awali ya mtu, mfumo wa neva unaodhibiti mwili na akili ya mtu, na taratibu za kiakili na kijamii. Baadhi ya dawa, zikiwemo dawa za kuagiziwa na daktari, zinaweza kusababisha dalili au kuzifanya mbaya zaidi. Utafiti wa hivi sasa unaangazia jukumu la mfumo wa neva ingawa hakuna mtu aliyepata kisababishi hata kimoja cha kiogani kilichojitenga. Miungano mingi ya dalili zinazoweza kutokea imepelekea mjadala kuhusu iwapo ugonjwa huu ni hali moja au hali nyingi tofauti. Neno "skizofrenia" linatokana na maneno mawili ya Griki yanayomaanisha "kugawanya" na "akili". Hata hivyo, skizofrenia haimaanishi "akili iliyogawanyika" wala kusababisha watu kuwa na nafsi nyingi (au "zilizogawanyika"). Watu wengi hushindwa kutofautisha skizofrenia na hali kama hizo.[3]
Matibabu hasa ni kwa kutumia dawa ili kupunguza dalili kuu. Dawa hizi husitisha nyendo katika sehemu za ubongo zinazochakata kemikali inayoitwa dopamine. (Baadhi ya dawa hizi pia husitisha shughuli katika sehemu ambazo huchakata kemikali inayoitwa serotonin.) Matibabu ambayo pia ni muhimu ni pamoja na therapi ya kiakili, usaidizi katika kutafuta na kudumisha kazi na pia marekebisho ya kimahusiano. Katika matukio makubwa ambapo kuna hatari kwa mtu binafsi na watu wengine, mtu anaweza kuhitaji kulazwa hospitalini. Hatua hii inaweza kuchukuliwa kwa idhini au bila idhini ya mtu huyu. Hata hivyo, matukio ya kulazwa hospitalini siku hizi yamepunguka na kuwa nadra ikilinganishwa na hapo awali.[4]
Skizofrenia hudhaniwa kuathiri hasa michakato ya kiakili, lakini pia huchangia matatizo ya muda mrefu pamoja na mwenendo na hisia. Watu walio na skizofrenia wana uwezekano wa kuwa na hali zingine pia, zikiwemo mfadhaiko na wasiwasi. Takriban asilimia 50 ya watu walio na skizofrenia hutumia madawa ya kulevya wakati mmoja maishani mwao.[5] Matatizo ya kijamii kama vile ukosefu wa kazi kwa muda mrefu, umaskini na ukosefu wa makao hutokea mara nyingi. Kwa wastani, watu walio na skizofrenia hufa miaka 12 hadi 15 mapema zaidi ya wale wasio na hali hii: Watu walio na skizofrenia wana matatizo ya mwili mengi zaidi, na wana kiwango cha uwezekano wa kujiua cha asilimia 5 zaidi ya watu wa kawaida.[2]