Spice Girls
kikundi cha muziki / From Wikipedia, the free encyclopedia
Spice Girls ni kundi maarufu la muziki wa pop kutoka nchini Uingereza. Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1994. Moja kati ya vibao vyao vikali ni pamoja na "Wannabe", "Spice Up Your Life" na "Stop".
Spice Girls | |
---|---|
Spice Girls wakiwa kazini | |
Maelezo ya awali | |
Asili yake | London, Uingereza |
Aina ya muziki | Pop rock, dance-pop, teen pop |
Miaka ya kazi | 1994–2001; 2007–2008 |
Studio | Virgin Records |
Tovuti | www.thespicegirls.com |
Wanachama wa sasa | |
Melanie Brown (Scary Spice) Victoria Beckham (Posh Spice) Emma Bunton (Baby Spice) Melanie Chisholm (Sporty Spice) Geri Halliwell (Ginger Spice) |
Kundi zima linaundwa na mwanachama kama: Victoria Beckham ("Posh Spice"), Melanie Brown ("Scary Spice"), Emma Bunton ("Baby Spice"), Melanie Chisholm ("Sporty Spice") na Geri Halliwell ("Ginger Spice").
Kundi limetoa albamu tatu: Spice mnamo mwaka wa 1996, Spice World mnamo mwaka wa 1997 na Forever mnamo mwaka wa 2000. The Spice Girls pia wamecheza kwenye filamu ya Spiceworld: The Movie, ambayo ilitolewa mnamo mwezi wa Desemba katika mwaka wa 1997.
Wasichana hao watano walikuja kuungana tena hapo mnamo mwaka wa 2007 na kutangaza kwamba wafanya ziara ya kimataifa Archived 24 Oktoba 2009 at the Wayback Machine. ambayo imeanza mwezi wa Desemba.