Alumini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Alumini ni elementi. Namba atomia yake ni 13 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 26.9815. Katika mazingira ya kawaida ni metali nyepesi yenye rangi nyeupe ya kifedha. Alama yake ni Al.
Ukweli wa haraka Alumini (aluminium) ...
Alumini (aluminium) | |
---|---|
Jina la Elementi | Alumini (aluminium) |
Alama | Al |
Namba atomia | 13 |
Mfululizo safu | Metali |
Uzani atomia | 26.9815 |
Valensi | 2, 8, 3 |
Densiti | 2.70 g/cm³ |
Ugumu (Mohs) | 2.75 |
Kiwango cha kuyeyuka | 933.47 K (660.32 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 2792 K (2519 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 7.57 % |
Hali maada | mango |
Funga
Alumini ni metali inayopatikana kwa wingi katika ganda la dunia.
Kutokana na densiti husianifu ndogo inatumiwa kila mahala ambapo wepesi ni muhimu, kwa mfano katika uundaji wa vitu mbalimbali kama utengenezaji wa ndege.