Awkwafina
Mwigizaji, mwimbaji na mchekeshaji wa Marekani / From Wikipedia, the free encyclopedia
Nora Lum[1] (anajulikana kitaaluma kama Awkwafina; amezaliwa Stony Brook, New York,[2] Juni 2, 1988)[3] ni mwigizaji, mwimbaji na mchekeshaji wa Marekani.
Awkwafina | |
---|---|
Amezaliwa | 2 June 1988 |
Utaifa | Mmarekani |
Majina mengine | Awkwafina |
Mhitimu | Chuo Kikuu cha Albany, SUNY (Shahada ya Sanaa) |
Kazi yake | Mwigizaji, Mwimbaji, Mtayarishaji wa Filamu |
Miaka ya kazi | 2005-hadi sasa |
Alipata umaarufu mnamo mwaka 2012 wakati wimbo wake uliyoitwa "My Vag" uliposambaa katika YouTube. Kisha alifuatia kutoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa Yellow Ranger (2014), na akawa akiigiza kwenye tamthilia zenye maudhui ya vichekesho iliyoitwa MTV Girl Code (2014-2015). Aliendelea na kuanza kuigiza katika filamu za vichekesho kama vile Neighbors 2: Sorority Rising (2016), Ocean's 8 (2018), Crazy Rich Asians (2018) na Jumanji: The Next Level (2019). Na baada ya kuigiza kama binti mwenye huzuni katika filamu ya The Farewell (2019) kulimfanya aweze kushinda Tuzo ya Golden Globe. Tangu 2020, Awkwafina amekuwa mtengenezaji, mwandishi, na mtayarishaji mkuu wa mfululizo wa tamthilia ya Vichekesho iliyoitwa Awkwafina Is Nora From Queens. Mnamo mwaka 2021, aliigiza kama Katy katika filamu ya Marvel Cinematic Universe Shang-Chi and Legend of the Ten Rings[4]. Pia ameigiza sauti katika filamu za katuni kama vile Storks (2016), The Angry Birds Movie 2 (2019), Raya and the Last Dragon (2021), The Bad Guys (2022), The Little Mermaid(2023), Migration (2023), na Kung Fu Panda 4 (2024).