Vijasumu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Vijasumu (kutoka Kiyunani βακτήριον, baktērion, yaani "kifimbo", kutokana na umbo la vijasumu vya kwanza kugundulika; pia: bakteria) ni viumbehai wadogo sana aina ya vidubini. Mwili wa vijasumu huwa na seli moja tu. Huonekana kwa hadubini tu na kwa sababu hiyo hawakujulikana katika karne za kale.
Bakteria | ||
---|---|---|
Bakteria aina ya Clostridium botulinum katika hadubini | ||
Uainishaji wa kisayansi | ||
| ||
Ngazi za chini | ||
Faili
Actinobacteria (ina guanini na sitosini nyingi)
Aquificae
Acidobacteria |
Kuna aina nyingi sana za vijasumu na idadi yao ni kubwa kushinda viumbe vingine vyote duniani.
Huishi kwenye ardhi na kwenye maji, ziko pia hewani zinaposukumwa na upepo.
Aina nyingi huishi ndani ya viumbe vikubwa zaidi. Mwanadamu huwa na bakteria nyingi ndani ya utumbo wake ambazo ni za lazima kwa mmeng'enyo wa chakula. Hata katika ngozi kuna bakteria nyingi ambazo zinakinga mwili dhidi ya vidubini vilivyo tishio. Lakini bakteria nyingine katika mazingira huweza kusababisha magonjwa na sehemu kubwa ya magonjwa ya kuambukiza yametokana na bakteria.
Bakteria huzaa kwa njia ya kujigawa na kuwa bakteria mbili ambazo ni sawa na seli asilia.