Belzebuli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Belzebuli (kwa Kiingereza: Beelzebub au Beelzebul, kutoka Kiebrania בַּעַל זְבוּב, Baʿal Zəvûv) ni jina lililotokana na lile la mungu mmojawapo wa Wafilisti wa Ekron, ambalo tena linahusiana na Baal, mungu mkuu wa Kanaani.
Baadaye lilitumiwa na Wayahudi, Wakristo na Waislamu kama jina la mmojawapo kati ya pepo wakuu zaidi, ila badala ya kumuita Beel Zebul, yaani Baal Mfalme, walitamka Baal Zebub, yaani mungu wa nzi[1][2][3][4][5][6][7].