Bonifasia Rodriguez
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bonifasia Rodriguez (jina kamili kwa Kihispaniaː Bonifacia Rodríguez y Castro; Salamanca, Hispania, 3 Juni 1837 - Zamora, Hispania, 8 Agosti 1905) alikuwa bikira mwanzilishi mwenza wa shirika la kitawa la Watumishi wa Mt. Yosefu ambalo ndani ya Kanisa Katoliki linahudumia wanawake fukara na wasio na ajira[1] wapate maendeleo ya kiroho na ya kijamii kwa njia ya sala na kazi[2].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 9 Novemba 2003, halafu Papa Benedikto XVI akatangaza mtakatifu tarehe 23 Oktoba 2011[3][4].