Dominiko wa Guzman
Padre wa Castilian na mwanzilishi wa Shirika la Dominika / From Wikipedia, the free encyclopedia
Dominiko wa Guzmán (Calaroga (Hispania) 1170 hivi - Bologna (Italia) 6 Agosti 1221) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki akaanzisha Shirika la Wahubiri ili kufufua mtindo wa maisha ya Mitume wa Yesu[1].
Mtu ambaye alikuwa anasema tu na Mungu au juu ya Mungu, alitangazwa mtakatifu na Papa Gregori IX tarehe 2 Julai 1234.