Eligius wa Noyon
From Wikipedia, the free encyclopedia
Eligius wa Noyon (kwa Kifaransa: Éloi; Chaptelat, Aquitaine, 588 hivi – Noyon, 1 Desemba 660) alikuwa sonara halafu mshauri mkuu wa mfalme wa Ufaransa Dagobati I.
Miaka mitatu baada ya kifo cha mfalme huyo, alichaguliwa kuwa askofu wa Noyon-Tournai (642). Hapo kwa miaka ishirini alijitahidi kufanya wakazi Wapagani wa Flandria waongokee Ukristo[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi[2] kama mtakatifu.