Fides wa Agen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fides wa Agen (alifariki Agen, Akwitania, leo nchini Ufaransa, 303 hivi) alikuwa mwanamke Mkristo aliyeuawa kwa ajili ya imani yake kutokana na dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakristo wa madhehebu mbalimbali kama mtakatifu mfiadini.