Gaudensi wa Rimini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gaudensi wa Rimini (Efeso, leo katika Uturuki, 280 hivi - Rimini, Italia, 14 Oktoba 360 BK) anakumbukwa kama askofu wa kwanza wa Rimini (Italia Kaskazini), aliyewajibika nyakati za dhuluma.
Wazazi wake walikuwa Wakristo waliomsomesha vizuri, ila wakaja kuuawa na wafuasi wa Mani. Hapo alihamia Roma (308) alipopata ubatizo halafu upadri (332) na uaskofu (346) akatumwa Rimini.
Huko, pamoja na maaskofu wa jirani alipinga uzushi wa Ario, mbali ya ibada za Upagani. Hatimaye aliuawa na Waario walioungwa mkono na kaisari[1].