Genoveva wa Nanterre
From Wikipedia, the free encyclopedia
Genoveva wa Nanterre (kwa Kifaransa: Geneviève; Nanterre, 411/416 - Paris, 3 Januari 512) alikuwa mtawa wa Ufaransa wa leo.
Alipokuwa na umri wa miaka 15, kwa shauri la Jermano askofu wa Auxerre, alijiweka wakfu kwa Mungu. Baadaye alifariji wakazi wa mji huo waliohofu uvamizi wa Wahunni, akawasaidia wakati wa njaa[1].